Kitendo cha
bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje mwaka 2018/19 kupitishwa leo mchana Mei 23,
2018 na kikao cha Bunge kuahirishwa hadi kesho, kimewagawa wabunge
Bajeti ya
wizara hiyo ya ShSh177bilioni iliyowasilishwa bungeni leo asubuhi na Balozi
Augustine Mahiga na kujadiliwa na wabunge wasiozidi 10, haikupata upinzani
kutoka kwa wabunge kama zilivyo bajeti nyingine tangu kuanza kwa Bunge la
bajeti Aprili 3, 2018.
Naibu Spika, Dk Tulia Ackson ameahirisha kikao hicho saa
7:45 mchana
Ilipofika saa
6:45 mchana, dakika 15 kabla ya muda wa kawaida wa kuahirisha kikao cha Bunge
hadi saa 10 jioni, Dk Tulia aliongeza nusu saa ili kutoa fursa kwa Balozi
Mahiga na Naibu wake, Dk Susan Kolimba kujibu hoja mbalimbali zilizotolewa na
wabunge
Baada ya
mawaziri hao kujibu, Bunge lilikaa kama kamati kupitisha bajeti hiyo,
baadaye Dk Tulia aliongeza tena nusu saa ambapo hakukuwa na mbunge aliyehoji
jambo lolote wakati wa kupitisha vifungu hivyo
Ilipofika saa
7:45 mchana, kikao hicho kiliahirishwa hadi kesho saa 3 asubuhi ambapo wabunge
mbalimbali waliozungumza na MCL Digital, wamekuwa na maoni yanayotofautiana.
Kauli za wabunge
Mbunge wa
Manonga (CCM), Seif Khamis Gulamali amesema, “hakuna agenda nyingine, shughuli
zilizopangwa kwa leo zimekwisha na kama unavyojua wizara hii huwa haina mambo
mengi, mahusiano yetu yako sawa kwa hiyo hakuna tatizo.”
Mbunge wa
Geita Mjini (CCM), Constantine Kanyasu amesema, “sijajua lakini nafikiri Dk
Tulia ameona orodha ya wachangiaji imekwisha, ndio maana akaongeza saa
moja na akamaliza.”
Mbunge wa
Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari amesema, “tulijiandaa kushika
vifungu na mpaka sasa hatujajua kwanini Bunge limemalizika muda huu maana
mbunge aliyechangia kwa upande wa Chadema alikuwa mmoja tu ambaye ni Sugu
(Joseph Mbilinyi-Mbeya Mjini).”
Nassari
anaungwa mkono na Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe, “mimi
mwenyewe sijui, sijui kuna nini. Nilijiandaa kukamata vifungu lakini imekwisha
haraka haraka, hatujajua kuna nini.”
Kwa upande
wake, Mbunge wa Ulanga (CCM), Goodluck Mlinga amesema Bunge si lazima
kuahirishwa jioni, kwamba shughuli za siku husika zinapokwisha na vikao
humalizika
“Unajua hii
wizara huwa si ngumu, ingekuwa wizara inayohusu mahindi au mifugo ungeona moto
wake. Kwa hiyo Dk Tulia ameona wachangiaji wameisha akaona aliahirishe Bunge
hadi kesho,” amesema mbunge wa Mbinga Mjini (CCM), Sixtus Mapunda.
Mbunge wa
Tanga Mjini (CUF), Mussa Mbarouk amesema, “mimi baada ya Naibu Spika kuongeza
nusu saa, nikatoka kwenda msikitini lakini wakati narudi naambiwa
limeahirishwa.”
“Unajua hii
wizara ina mambo mengi tunajadili mustakabali wa Tanzania nje ya nchi, sasa
kuijadili kwa muda mfupi sijajua kuna nini na sijajua kwa nini imepelekwa
haraka haraka hivi.”
Bajeti Wizara ya Mambo ya Nje yapitishwa
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 23, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 23, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment