Mahakama Kuu
Kanda ya Dar es Salaam leo Mei 23, 2018 imemwamuru mkurugenzi wa kampuni ya
Tiptop Connections, Hamis Shaban Taletale maarufu Babu Tale, kukaa mahabusu
katika kituo cha Polisi akisubiri amri ya kupelekwa kifungoni katika Gereza la
Ukonga
Mahakama hiyo
katika uamuzi uliotolewa na Naibu Msajili, Wilbard Mashauri Februari 16, 2018,
iliamuru Babu Tale na ndugu yake Idd Shaban Taletale wakamatwe na kupelekwa
kifungoni katika gereza la Segerea baada ya kushindwa kutekeleza hukumu yake
Katika hukumu
hiyo iliyotolewa na Jaji Agustine Shangwa Februari 18, 2016, iliwaamuru ndugu
hao kumlipa fidia ya Sh250 milioni, Mhadhiri wa Dini la Kiislam Sheikh Hashim
Mbonde, kutokana na makosa ya kutumia mahubiri yake kibiashara bila ridhaa yake.
Kutokana na amri hiyo ya kuwakamata, Babu Tale
alitiwa mbaroni jana na kupelekwa mahakamani hapo kwa ajili amri ya kumpeleka
kifungoni, lakini alilazimika kurudishwa mahabusu Kituo Kikuu cha Polisi kwa
kuwa Naibu Msajili aliyetoa amri ya kuwakamata hakuwapo
Leo amri ya
kumrejesha rumande ilitolewa na Naibu Msajili wa mahakama hiyo, Ruth Massam,
mpaka Naibu Msajili Mashauri aliyetoa amri ya kuwafunga atakaporejea kutoka
Dodoma alikokwenda kikazi.
Kwa kuwa haijulikani ni lini atarejea, Babu
Tale atalazimika kukaa mahabusu kwa muda usiojulikana mpaka Naibu Msajili
Mashauri atakaporejea
Mahakama yampeleka Babu Tale mahabusu kwa muda usiojulikana
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 23, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 23, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment