Mkazi wa kijiji cha Malumba
wilayani Tunduru mkoani Ruvuma Zuberi Mahochi ameuawa kwa kushambuliwa na
Tembo wakati akijaribu kumfukuza Tembo katika shamba lake katika kijiji cha
Misyaje jirani na hifadhi ya wanyamapori ya Chingoli huku vijiji vitano vikizingirwa
na Tembo na kusababisha wananchi waishi kwa hofu wilayani humo.
Akizungumza ndugu wa
marehemu ambaye ni mama mdogo wa marehemu Fatma Ally pamoja na kuzungumzia
masikitiko ya kumpoteza ndugu yake anaiomba serikali kuwalinda dhidi ya tembo
kwa kuwa wanaishi kwa hofu
|
|
Vijiji vitano vinavyosumbuliwa na
Tembo ni kijiji cha Masyaje kulikotokea kifo ,Mkowela,Hulia Makande na
kijiji cha Rahaleo na hapa mwenyekiti wa kijiji cha Mkowela Bw.
Suleiman Somanga anasema wananchi mbali na kupoteza mazao yao lakini
wanaishi kwa hofu ya kuuawa na Tembo
|
|
Mkuu wa wilaya ya Tunduru
Bw. Juma Homera aliyetembelea eneo la tukio na kushiriki maziko
ya marehemu Mahochi anasema kuwa serikali kwa kushirikiana na idara ya
wanyamapori,mamlaka inayoshughulikia wanyamapori(TAWA),kikosi dhidi ya
ujangiri(KDU)Pams foundation wanawarejesha Tembo kwenye hifadhi
|
Mtu mmoja auawa kwa kushambuliwa na Tembo wilayani Tunduru
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 23, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment