Serikali inamikakati ya kuhakisha
wahitimu wa vyuo wanapata ajira za kuajiriwa na kujiajiri ambapo moja ya
mikakati hiyo ni kusimamia utekelezaji wa sera ya uchumi wa viwanda
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri
Ofisi ya Waziri Mkuu,Ajira,Kazi na Vijana Anthony Mavunde wakati akijibu
swali la Mhe.David Silinde Mbunge wa Momba aliyetaka kujua mikakati ya
serikali katika kuongeza ajira.
|
|
Mh Mavunde akasema kuwa serikali
inatekeleza miradi mikubwa nchini ikiwemo mradi wa bomba la mafuta,ujenzi wa
reli ya kisasa na ujenzi wa miundombinu ya usambazaji wa nishati
kupitia miradi mbalimbali ambayo yote kwa ujumla itasaidia kupanua wigo
wa nafasi za ajira
|
|
Aidha akaongeza mkakati mwingine
ni kuendeleda kuwezesha vijana kujiajiri kwa kuwapatia mikopo yenye
msharti nafuu kupitia mfuko wa maendeleo ya vijana
|
|
Mh Mavunde akasema kuwa serikali
itaendelea kusimamia utekelezaji wa program ya taifa ya kukuza ujuzi ambayo
itasaidia kwa kiasi kikubwa kuwezesha vijana kuajirika na kupunguza
tofauti ya ujuzi iliyopo kati ya nguvu kazi na mahitaji ya soko la
ajira.
|
Serikali kuhakikisha wahitimu wa vyuo wanapata ajira.
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 23, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment