Serikali
mkoani Tanga imewaagiza wakuu wilaya na wakurugenzi wa halmashauri kuhakikisha
kuwa wanawachukulia hatua kali za kisheria baadhi ya watendaji wao baada ya
kubaini kuwa baadhi yao wanapokea mishahara ya watumishi hewa waliostaafu huku
wengine wakiwa wamefariki dunia na kuzorotesha zoezi la Mheshimiwa rais
Dkt.John Pombe Magufuli la kukabiliana na matumizi mabaya ya fedha za
serikali.
Akizungumza na viongozi wote wa
serikali za mkoa wa Tanga mkuu wa mkoa wa Tanga Martin Shigella amesema
inastaajabisha baadhi ya mishahara hiyo bado inaendelea kutumika halafu
watendaji husika wanashindwa kuchukua hatua kali za kisheria hivyo ni lazima
fedha hizo zirudishwe
|
|
Aidha amesema wamebaini kuwa bado
wapo baadhi watendaji wa halmashauri ambao wanakusanya maduhuli ya serikali
wanadaiwa kuficha vitabu vya makusanyo hatua aliyoielezea kuwa ni yenye
ishara ya hujuma
|
|
Kufuatia hatua mkurugenzi
halmashauri ya wilaya ya Muheza Luiza Mlelwa amekiri kuwepo kwa mishahara
hewa inayoingizwa kwenye benki wanazochukua mishahara watumishi na wamejaribu
kuwaandikia viongozi wa benki ili kurudisha fedha hizo makao makuu hazina
lakini hadi sasa ameshindwa kujibiwa.
|
Watumishi hewa walipwa mishahara Tanga
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 23, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment