Serikali kupitia wizara ya afya imeweka wazi
mpango wake wa kufanya tathimini nchini nzima ili kujua idadi kamili ya
wanawake wanaokabiliwa na wagonjwa wa fistula ili kuweza kurahisisha uratibu
wa matibabu ya upasuaji kwa wagonjwa hao ambao wengi wao wako pembezoni mwa
nchi
|
Watalaam wa afya wanasema moja ya visababishi vya
ugonjwa wa fistula ni uzazi pingamizi, na mimba za utotoni ambapo kwa mwaka
2016 pekee zaidi wanawake wenye fistula 1000 walipatiwa matibabu na kwa
mujibu wa UNFPA wanasema matukio ya fistula 1200 hadi 3000 yamekuwa
yakiripotiwa hapa nchini huku wadau wa afya wakisema ni muhimu huduma za afya
ya mama na mtoto zikazidi kuimarishwa hasa maeneo ya pembezoni mwa nchi
|
Serikali inasema ni muhimu kwa wanawake wajawazito
kujifungulia katika vituo vya afya ikiwa ni pamoja na kuhudhulia cliniki kwa
wakati ambapo sasa tayari vituo vya afya 200 zimeanza kufanyiwa ukarabati ili
kutoa huduma za mama na mtoto kote nchini
|
Kila ifikapo May 23 kila mwaka Tanzania huungana na
nchi zote ulimwenguni kuadhimisha siku ya fistula lengo ikiwa ni kuhakikisha
jamii inaondoka na dhana ya unaynyapaa kwa wagonjwa wa fistula ambayo sasa
inatibika pasi na gharama yoyote
|
Serikali kufanya tathimini ya wagonjwa wa Fistula nchini.
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 23, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment