Mkurugenzi wa
Kampuni ya Tip Top Connection ya jijini Dar es Salaam, Hamis Taletale maarufu
Babu Tale, leo Mei 23, 2018 saa 6 mchana amefikishwa Mahakama Kuu Kanda ya Dar
es Salaam kusikiliza kesi inayomkabili, akiwa chini ya ulinzi wa polisi.
Babu Tale, ambaye pia ni meneja wa mwanamuziki
maarufu wa 'Bongo Fleva' Diamond Platnumz, alikamatwa kufuatia amri iliyotolewa
Februari 16, 2018 na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda Maalum, Wilbard
Mashauri iliyoelekeza kukamatwa mtuhumiwa huyo na ndugu yake, Idd Taletale
Amri hiyo pia,
ilielekeza watakapokamatwa wapelekwe Gereza la Ukonga wakiwa wafungwa wa kesi
ya madai, hadi hapo mahakama hiyo itakapotoa maelekezo mengine
Hata hivyo,
Babu Tale hakuweza kupatikana na ndipo mahakama hiyo ikatoa amri nyingine kama
hiyo Aprili 4 mwaka huu. Tangu hapo wamekuwa wakitafutwa bila mafanikio hadi
jana alipokamatwa
Mahakama hiyo
iliwaamuru kumlipa Mhadhiri wa Dini ya Kiislamu, Sheikh Hashim Mbonde
kiasi cha Sh250 milioni, baada ya kupatikana na makosa ya ukiukwaji wa haki za
hakimiliki kwa kutumia masomo yake kibiashara bila ridhaa yake kinyume cha
Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki
Leo baada ya
kufika mahakamani mbele ya Naibu Msajili, Ruth Massam, amewapa muda wa dakika
10 pande zote wajadiliane namna ya kulimaliza suala hilo
Babu Tale yupo
mahabusu ya mahakama hiyo wakati ndugu zake wanajadiliana na mdai wake kabla ya
kuieleza mahakama muafaka watakaofikia na kisha mahakama kutoa maelekezo.
Katika kesi ya msingi, Sheikh Mbonde alikuwa
akidai kuwa aliingia mkataba na kampuni ya kina Babu Tale (Tiptop Connection)
ili wamrekodi mahubiri yake kisha wayauze na kugawana mapato.
Hata hivyo
baada ya kurekodi masomo saba, walimkatia mawasiliano na alipowatafuta na
kukutana nao wakamweleza kuwa wameamua kuachana na mpango huo.
Sheikh Mbonde alidai kuwa akiwa kwenye
mahubiri Dodoma ndipo akakutana na mikanda ya video katika mfumo wa DVD yenye
mahubiri yake huku kukiwa na namba za simu za viongozi hao wa Tiptop
Sheikh Mbonde
alidai baada ya kufanya uchunguzi alibaini kuwa DVD hizo zilikuwa zikiuzwa
katika mikoa mbalimbali, ndipo akawafungulia kesi ya madai ya fidia kutokana
ukiukwaji wa Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki
Meneja wa Diamond Babu Tale afikishwa kortini
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 23, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 23, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment