Mbunge wa
Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi maarufu Sugu amesema suala la Rais John
Magufuli kusafiri nje ya nchi haliepukiki
Akizungumza
katika mjadala wa bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje, Afrika Mashariki, Kikanda
na Kimataifa ya mwaka 2018/19 bungeni mjini Dodoma, Sugu amesema kuna
mikutano inayopaswa kuhudhuriwa na rais mwenyewe, si kuwakilishwa na Makamu wa
Rais na Waziri Mkuu
Hata hivyo,
Rais Magufuli amewahi kueleza kuhusu safari zake, kubainisha kuwa hakuchaguliwa
na Watanzania ili kusafiri nje ya nchi.
Magufuli
ametembelea Kenya, Uganda, Rwanda na Ethiopia katika kipindi chote cha utawala
wake huku akitimiza takribani miaka miwili na nusu tangu aapishwe kuwa Rais wa
Tanzania Novemba 5, 2015
Machi mwaka
huu Rais Magufuli akiwa mjini Singida katika uzinduzi wa kiwanda cha mafuta ya
kupikia cha Mount Meru Millers Group, alisema amekataa zaidi ya mialiko 70 ya
kwenda nje ya nchi kwa sababu hakuchaguliwa na Watanzania kwenda huko bali
kuwatumikia
Amesema jimbo
lake ni Tanzania na kwamba hawezi kwenda wakati hajamaliza kutatua kero za
wananchi waliompigia kura na wabunge wa chama chake CCM
“Suala la
kusafiri bado ni muhimu, tena anapokwenda nje anaweza kutumia lugha ya
Kiswahili kwa sababu Rais Xi Jinping wa China kila anapokwenda anaongea
kichina licha ya kuwa msomi na anazungumza Kiingereza,” amesema Sugu
“Kama tatizo
ni gharama, mbona anatuma delegation (ujumbe) mara makamu wa rais, mara
waziri mkuu nao wanatumia gharama kwa sababu hawaendi kule kwa miguu, sasa
hatuendi UN (Umoja wa Mataifa), Davos, Commonwealth.”
>Sugu
ambaye hivi karibuni alitoka gerezani kwa msamaha wa Rais amesema, “mikutano ya
common wealth (Jumuiya za Madola) ni ya wakuu wa nchi lakini sisi tunatuma
wawakilishi, kuna fursa za kiuchumi na kibiashara.”
Rais Uhuru
Kenyatta (wa Kenya) ametumia vizuri sana fursa za uchumi na kibiashara
kwa nchi yake alivyokwenda pale hali kadharika Rais wa Afrika Kusini nae
anatumia fursa.”
Amesema
kutokana na fursa hizo, rais kusafiri nje hakuepukiki, “ni kama alivyonukuliwa
mzee Kikwete (Jakaya-Rais wa Serikali ya Awamu ya Nne) aliposema kusafiri
kumemsaidia sana kwani mkaa bure si sawa na mtembea bure.”
Sugu ahoji safari za Rais Magufuli nje ya nchi
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 23, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 23, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment