Mbunge wa Kigoma Mjini
(ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe amemtaka Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi
Kigwangalla kukubali amekosea na kurejea katika utaratibu wa awali wa utoaji wa
vibali vya vitalu vya uwindaji
Akichangia bajeti ya wizara hiyo ya
mwaka 2018/19 ambayo ni Sh115.8bilioni, Zitto amesema:, “Waziri kwa kuwa umeona
kuna tatizo la kisheria na maagizo uliyoyatoa ni kinyume na sheria turejee
katika utaratibu wa awali.”
Zitto ambaye pia ni Kiongozi wa ACT-Wazalendo
amesema hakuna anayepinga nchi kuongeza uwezo wa uzalishaji wa umeme, “Lakini
tunataka taratibu za sheria zifuatwe. Kitendo cha kukata miti zaidi ya 1,400
katika hifadhi ya Selous ukubwa sawa na jiji la Dar es Salaam kweli, kila
mbunge afumbe macho hapa aitizame Dar es Salaam isiyo na miti.”
“Lengo la wizara ifikapo mwaka 2025
ni nchi kuwa na watalii milioni nane kwa mwaka na kuingiza dola bilioni 16 za
Marekani, ukienda kuiondoa selous yote huwezi kuifikia huku?”
Huku akizungumzia uzalishaji wa
umeme wa gesi ulivyo gharama amesema, “Lakini kuzalisha kwa maji inatuchukua
muda, suala la TFS (Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania) kwenda kuangusha miti
si sahihi. Jambo hili lisimame mpaka tathimini ya mazingira itakapofanyika.
Tunakwenda kupotea njia kabisa ya kukuza utalii. Mheshimiwa Spika hebu
litizameni hili kwa upana wake.”
Zitto amshukia Kigwangalla
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 22, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 22, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment