|
Mbunge wa Mbeya Mjini
Joseph Mbilinyi 'Sugu' amelitetea Jeshi la Magereza mbele ya
Bunge kuwa jeshi hilo lina matatizo makubwa ya kiusafiri jambo ambalo
linapelekea wafungwa kupelekwa Mahakamani kwa miguu kitendo ambacho kina
hatarisha usalama wa mfungwa na askari kiujumla.
Kauli hiyo ya Sugu imetolewa leo
Mei 22, 2018 Bungeni Jijini Dodoma kwenye kikao cha 34 mkutano wa 11 wa Bunge
la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati wa kipindi cha maswali na
majibu kwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
"Pamoja na matatizo
waliyokuwa nayo Jeshi la Polisi katika masuala ya vyombo vya usafiri lakini
niwahakikishie Jeshi la Magereza lina hali mbaya sana, hawana magari sio tu
magari mabovu hawana magari kabisa, kiasi kwamba wanafikia hatua ya kuwapeleka
wafungwa ambao wanakesi Mahamani kwa miguu huku wakiwa wamewafunga pingu. Hii
ni mbaya sana kwa usalama wa askari magereza pamoja na wale watuhumiwa ambao
wamefungwa pingu", amesema
Sugu.
Pamoja na hayo, Sugu ameendelea
kwa kusema "mtu anatuhumiwa ujambazi halafu anapitishwa
mtaani kwa miguu wananchi wanamuona, wanaweza wakamvamia na kumshambulia
pamoja na kuhatarisha maisha ya mfungwa".
Kutokana na ushauri huo, Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mwigulu Nchemba akampongeza Mhe. Sugu kwa
kusema "nimpongeze Mhe. Sugu kwa kuuliza swali kwa
experience, na niseme kwamba yeye ni mshauri mzuri. Tutalizingatia hilo ili
tuweke mgao kwenye upande wa Jeshi la Magereza ili kuepuka na tahadhari
aliyosema".
|
|
Sugu alitetea Jeshi la Magereza
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 22, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 22, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment