Nape aitaka Serikali kuheshimu sheria

Mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye amemtaka Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuisaidia Serikali kujenga utamaduni wa kuheshimu sheria zinazopitishwa na Bunge

Akizungumza bungeni leo Mei 22, 2018 katika mjadala wa bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii mwaka 2018/19, Nape amesema wakati wakikamilisha kuandaa taarifa ya kamati kuhusu bajeti hiyo, Wakala Huduma za Misitu Tanzania (TFS) walitangaza zabuni ya kukata miti katika pori la Selous

Amesema ukubwa waliotangaza miti itakapokatwa ni kama ukubwa wa Jiji la Dar es Salaam na wapo wanaosema ukubwa huo unalingana na kisiwa cha Unguja, Zanzibar

Amesema hifadhi hiyo ni kubwa nchini na kutangazwa kwa tenda hiyo kumeshtua

Hata hivyo,  amesema sheria ya usimamizi wa mazingira sehemu ya saba inatamka kuwa maeneo yatakayogundulika kuwa na madini na maji kufanyiwa tathmini ya mazingira kabla ya mradi kufanyika, lakini TFS imetangaza zabuni hiyo wakati  tathmini haijakamilika
Amesema tathmini hiyo ni muhimu kwa utambuzi wa hali halisi ya mazingira na jamii inayozunguka eneo husika: 

“Mwanasheria Mkuu wa Serikali aisaidie Serikali kujenga utamaduni wa kuheshimu na kwa unyenyekevu mkubwa naomba isitishe zoezi isubiri kwanza tathmini ya kimkakati ya kimazingira.”

Amesema msitu huo unazunguka na mikoa mitano ya Morogoro, Pwani, Lindi, Mtwara na Ruvuma na kwamba haiwezekani kupuuza jambo hilo.
Nape aitaka Serikali kuheshimu sheria Nape aitaka Serikali kuheshimu sheria Reviewed by KUSAGANEWS on May 22, 2018 Rating: 5

No comments: