|
Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema
wahifadhi wamekuwa ni walafi mno wa ardhi kwa kutaka maeneo makubwa nchini
Amesema hayo bungeni leo Jumanne
Mei 22, 2018 baada ya mbunge wa Muleba Kusini (CCM), Profesa Anna Tibaijuka
kuchangia katika bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa mwaka wa fedha
2018/19
Ndugai amesema wanapokwenda watu
wa hifadhi wanakuwa na wataalamu kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo
ya Makazi ambao hupima ardhi baada ya kukubaliana na wananchi
Hata hivyo, Ndugai amesema
wakati wanaporudi ofisini wanaongeza eneo bila kuwataarifu wananchi na
baada ya miaka 10 hupita maeneo husika na kuwaeleza kuwa mpaka upo
maeneo mengine
“Si waseme (wawambie wananchi)
mimi mwenyewe ni mhifadhi tatizo sisi wahifadhi ni walafi mno wa ardhi,”
amesema
Awali, Profesa Tibaijuka akichangia
amemweleza Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla kuwa yeye
(Kigwangalla) ni daktari wa binadamu na kwake ni kulinda maisha ya watu,
lakini kwenye masuala ya hifadhi kunamuangusha kutekeleza umuhimu huo
“Rais wetu anawalinda wanyonge
lakini majirani wa hifadhi si wanyonge. Kusema ukweli hali ilivyo si hivyo,”
amesema
Amemshauri Dk Kigwangalla kuachana
na misitu ya akiba na mapori ya akiba, kwa sababu yamepitwa na wakati badala
yake atangaze Hifadhi ya Taifa ambayo ina manufaa makubwa
Amesema wizara hiyo haina mamlaka
ya kupima ardhi
bali jukumu lipo kwa Wizara ya
Ardhi lakini katika uwekezaji wa mipaka wameenda bila kuwa na watalaamu wa
wizara hiyo
Ametoa mfano wa Msitu wa Kazimzumbwi ambao
Wizara ya Maliasili ilibadilisha mipaka na kusababisha mgogoro
Pia, Profesa Tibaijuka ameshauri
wizara hiyo kuachana na operesheni kwa sababu ni mambo ya haraka na ya
kushtukiza
|
|
Ndugai awapa makavu wahifadhi
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 22, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 22, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment