Sugu atinga bungeni na nembo ya namba yake ya mfungwa


Siku 12 tangu Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ alipoachiwa huru, jana aliingia bungeni na kusimamisha shughuli za Bunge kwa dakika kadhaa

Sugu, ambaye ni mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), alihudhuria kikao cha 33 cha Bunge la Bajeti lililoanza Aprili 3 likitarajiwa kuhitimishwa Juni 29 akiwa amevaa suti ya bluu bahari ikiwa na nembo ya namba yake ya mfungwa 219/2018.

 Akiwa ameongozana na mbunge wa viti maalumu (Chadema), Kunti Yusuph, Sugu alikanyaga lango la kuingia bungeni saa 3:16 asubuhi kabla ya kuingia ukumbini saa 3:20

Wakati akiingia, mbunge huyo alipita katikati ya ukumbi na wabunge wa upinzani walianza kumshangilia kwa kugonga meza. Awali alikosa vikao vya Bunge tangu Novemba, mwaka jana

Wa kwanza kusalimiana na mbunge huyo alikuwa mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye kisha akapokewa na mbunge wa Rombo (Chadema), Joseph Selasini kwa upande wa upinzani.
Sugu atinga bungeni na nembo ya namba yake ya mfungwa Sugu atinga bungeni na nembo ya namba yake ya mfungwa Reviewed by KUSAGANEWS on May 22, 2018 Rating: 5

No comments: