Serikali
imeanza kutekeleza miradi ya maji kutoa maziwa makuu nchini kupeleka kwa
wananchi wanaoishi karibu na maziwa hayo.
Kauli hiyo
imetolewa leo Jumanne Mei 22, 2018 na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa
Aweso wakati akijibu swali la mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Silafu
Jumbe Maufi aliyehoji Serikali kama haioni umuhimu wa kuanzisha mradi wa maji
kutoka kwenye vyanzo hivyo na kusambaza kwa wananchi
Katika
ufafanuzi wake naibu waziri huyo amesema Serikali itaendelea na jitihada
za kutumia vyanzo vya maji vya Ziwa Rukwa kwa ajili ya kuhudumia wananchi wa
mikoa ya Katavi, Rukwa na Kigoma.
“Hivyo Wizara imeziagiza mamlaka za majisafi
na usanifu wa miradi ya maji na uandaaji wa makablasha ya zabuni kwa ajili ya
miradi ya maji itakayotumia vyanzo hivyo,” amesema Aweso
Kwa mujibu wa
naibu waziri huyo, amesema utekelezaji wa miradi hiyo unafanyika kupitia
programu ya maendeleo ya sekta ya maji awamu ya pili ya (WSDP II).
Mradi wa maji kutoka Ziwa Tanganyika kukamilika Juni mwaka huu
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 22, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 22, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment