Mkoa wa Kagera umetajwa kuwa na upungufu wa vyumba vya
madarasa 8,341 vya shule za msingi sawa na asilimia 58, Bunge limeelezwa leo
Jumanne Mei 22, 2018. Mkoa huo una mahitaji ya vyumba vya madarasa 14,275
lakini vilivyopo ni 5,934.
Akizungumza bungeni
leo Naibu Waziri wa Tamisemi, Josephat Kandege amesema kuwa katika mkoa huo pia
kuna mahitaji ya ofisi za walimu 1,780, kwamba zilizopo ni 925 na hivyo kuwa na
upungufu wa ofisi 855 ambayo ni asilimia 48
Kandege ametoa kauli hiyo wakati akijibu swali la mbunge wa
Viti Maalum (CUF), Alfredina Kahigi aliyetaka kujua Serikali inawasaidiaje
wanafunzi wa mkoa huo kupata mahali pazuri pa kusomea pamoja na walimu kupata
ofisi nzuri ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi mkubwa.
Katika maelezo yake
naibu waziri huyo amesema kwa shule za sekondari kuna mahitaji ya vyumba
vya madarasa 2,379, vilivyopo ni i 1,582.
“Kwa sekondari kuna upungufu wa vyumba 797 vya
madarasawa sawa na asilimia 34. Majengo ya utawala yanayohitajika ni 212,
yaliyopo sasa ni 67 na hivyo kusababisha upungufu wa majengo 145 ambao ni
asilimia 68,” amesema.
Naibu Waziri amesema upungufu pia umejitokeza katika
miundombinu mingine zikiwemo nyumba za walimu, vyoo na maabara na tayari
Serikali imefanya mikakati mbalimbali kuhakikisha kuwa wanafunzi na walimu
katika mkoa huo na Taifa wanapata mahali pazuri pa kusomea
Kagera kuna upungufu wa vyumba vya madarasa 8,341
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 22, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 22, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment