Chama cha Wananchi (CUF) Zanzibar kimetoa onyo kali kwa
wanachama ambao ni wajumbe wa mkutano mkuu Taifa kutoshirikiana na waliowaita
wasaliti wa chama hicho
Akizungumza na gazeti hili jana, mkurugenzi wa habari uenezi
na uhusiano wa umma upande wa katibu mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad,
Salim Bimani alisema wameshatoa tamko kuwataka wajumbe wa mkutano mkuu Taifa
kukataa kurubuniwa ili kushiriki mkutano huo
Bimani alisema tayari wana tetesi kuwa mkutano huo
unaratibiwa na CUF Lipumba
Alisema chama chao kina wajumbe wa mkutano mkuu halali
kupitia mabaraza ya wilaya upande wa bara na visiwani
“Hapa nataka niweke wazi hatutamvumilia mwanachama yeyote
yule ambaye ni mjumbe wa mkutano mkuu Taifa kuona anashirikiana na Lipumba na
kundi lake, ndiyo maana tumetoa tamko hili mapema kupitia wilaya zote kuwataka
wanachama wetu kutoshiriki kwa namna yoyote ile,’’ alisema Bimani
Alidai kuwa mkutano huo mkuu unaratibiwa kwa ajili ya
kumuondoa Maalim Seif kwenye nafasi yake ya ukatibu mkuu
Hata hivyo, naibu mkurugenzi wa uchaguzi wa CUF Lipumba,
Nassor Seif alisema kwa mujibu wa katiba ya chama chao mkutano mkuu huitishwa
na baraza kuu la chama, hivyo iwapo baraza hilo litakaa na kuona ipo haja ya
kuitishwa kwa mkutano huo basi hakuna wa kuzuia
Seif alisema kwa mujibu wa katiba yao mkutano mkuu unaweza
kufanyika kila mwaka kinyume na ilivyozoeleka sasa ndani ya chama hicho,
hufanyika kila baada ya miaka mitano.
Alisema mabadiliko ya
muda wa mkutano huo hutokea kulingana na sababu za fedha
“Acheni kuishi kwa ndoto kwani kila mmoja anafahamu ukweli
uliopo hivi sasa kuhusu nani anafuata katiba ya chama na nani hafuati,” alisema
Seif
CUF Maalim yashtukia janjanja CUF Lipumba
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 22, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 22, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment