Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe
(ACT-Wazalendo), amemtaka Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla
kukubali amekosea na kurejea katika utaratibu wa awali wa utoaji wa vibali vya
vitalu vya uwindaji.
Akichangia bajeti ya wizara hiyo ya
mwaka 2018/19 ambayo ni Sh115.8bilioni, Zitto amesema:, “Waziri kwa kuwa umeona
kuna tatizo la kisheria na maagizo uliyoyatoa ni kinyume na sheria turejee
katika utaratibu wa awali.”
Zitto katika hatua nyingine ametoa
wito kwa wizara husika kutafakari upya suala la kuondoa miti katika hifadhi ya
Sealou kwani kwa kufanya hivyo kutaathiri mazingira kwa kiasi kikubwa.
“Hakuna anayekataa maendeleo ya
taifa letu lakini kwa kuondoa miti ile kutaathiri mazingira pamoja na kupoteza
watalii, tunaomba zoezi hili lisimame kwanza tutafakari athari zake ndio uamuzi
ufanyike”. Amesema Zitto.
Zitto amkosoa Kigwangalla
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 22, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 22, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment