Aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mjini
Magharibi Visiwani Zanzibar, Hassan Nassir Ali, amefunguka juu ya uhamisho wake
aliopewa siku chache baada ya kuwaonya wanaume juu ya tabia zao zisizofaa
kwenye jamii.
Akizungumza, Kamanda Hassan amesema
kwamba uhamisho wake ni wa kawaida na wala haujatokana na kauli alizotoa,
ambazo zilizua gumzo kwenye mitandao ya kijamii.
Akiendelea kutolea ufafanuzi suala
hilo Kamanda Hassan amesema kwamba kauli hiyo aliitoa na alikuwa anamaanisha,
lakini haijaleta mtafaruku wowote kwenye jamii kama ambavyo inasemekana, na
hata walipoijadili kwenye Baraza la Wawakilishi Zanzibar ilikuwa ni utani.
“IGP amesema mwenyewe amefanya
uhamisho na uteuzi huu ili kuimarisha safu yake kiutendaji, mimi ningekuwa
nimesema nimewakwaza watu sio kweli, hata wale waliosema katika Baraza la
Uwakilishi ilikuwa ni kwa utani, ni uhamisho wa kawaida kabisa, wala sio
chuki”, amesema Kamanda Hassan.
Kamanda Hassan ameendelea kwa
kuwataka wananchi wa Kaskazini Pemba ambako amehamishiwa kufuata sheria
bila shuruti kwani kazi iko pale pale.
“Nitaendelea kufanya kazi yangu
vizuri nitaendelea kusimamia sheria vizuri, kazi iko pale pale bado mimi ni
Kamanda wa polisi nitasimamia sheria za nchi, wala sio jambo langu hili wala
mie sio mzee wa vikohozi, mimi nimetoa mifano, hivyo kazi iko pale pale”,
amesema Kamanda Hassan.
Kamanda huyo ambaye metokea visiwani
Zanzibar wiki iliyopita aliibua mzozo kwenye mitandao baada ya kuwaonya wanaume
wenye tabia ya kukohoa pindi waonapo wanawake wenye maumbile makubwa, akisema
hilo ni kosa kisheria ambalo linatambulika kama shambulio la aibu.
Kamanda aliyewaonya wanaume azungumzia kuhamishwa
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 22, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 22, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment