Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dkt.
Khalfan Haule amethibitisha kufariki kwa wagonjwa saba wa kipindupindu katika
Wilaya ya Sumbawanga huku wagonjwa wengine 44 wakibaki wodini kuendelea
kupatiwa matibabu na wagonjwa 115 wakiruhusiwa kurudi nyumbani.
Akizingumzia tukio hilo Dkt. Haule
amesema kuwa ugonjwa huo umelipuka Mei 6, 2018 katika Kijiji cha Mayenje, kata
ya Milepa katika bonde la Ziwa Rukwa na kusambaa katika maeneo mengine ya
Wilaya na hatimaye kupatikana kwa wagonjwa wawili katika hospitali ya rufaa ya
mkoa.
"Sasa hivi katika bonde la ziwa
Rukwa kuna shughuli za uvunaji wa mpunga na hivyo watu wengi hutokea huku juu
kwenda bondeni kutafuta vibarua vya kuvuna mpunga kwenye maeneo hayo
yaliyoathirika na kipindupindu, maji yanayotumika huko ni machafu kutoka katika
madimbwi na mito. Nawaomba viongozi wa dini watoe tahadhari kwa waumini hasa
katika maeneo yale yalioathirika zaidi", amesema Dkt. Haule.
Watu 7 wafariki Sumbawanga, 44 walazwa hospitalini
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 22, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 22, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment