Mkurugenzi wa Kampuni ya Tip Top Connection ya jijini Dar es
Salaam, Hamis Taletale maarufu Babu Tale, ametiwa mbaroni na
kufikishwa mahakamani na Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam kwa amri ya
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam
Babu Tale amekamatwa kufuatia amri iliyotolewa Februari 16,
2018 na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda Maalum, Wilbard Mashauri
iliyoelekeza kukamatwa mtuhumiwa huyo na ndugu yake, Idd Taletale
Amri hiyo pia, ilielekeza watakapokamatwa wapelekwe Gereza
la Ukonga wakiwa wafungwa wa kesi ya madai, hadi hapo mahakama hiyo itakapotoa
maelekezo mengine
Hata hivyo, Babu Tale hakuweza kupatikana na ndipo mahakama
hiyo ikatoa amri nyingine kama hiyo Aprili 4 mwaka huu. Tangu hapo wamekuwa
wakitafutwa bila mafanikio hadi jana alipokamatwa
Mahakama hiyo iliwaamuru kumlipa Mhadhiri wa Dini ya
Kiislamu, Sheikh Hashim Mbonde kiasi cha Sh250 milioni, baada ya kupatikana na
makosa ya ukiukwaji wa haki za hakimiliki kwa kutumia masomo yake kibiashara
bila ridhaa yake kinyume cha Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki
Baada ya kutiwa mbaroni leo alifikishwa mahakamani saa tisa
alasiri kwa ajili ya hatua zaidi. Hata hivyo, Naibu Msajili wa
Mahakama hiyo, aliyetoa amri ya kumkamata hakuwepo. Kufuatia kutokuwepo
kwa msajili huyo Taletale amerudishwa mahabusu Kituo Kikuu cha Polisi hadi
kesho asubuhi atakapopelekwa tena mahakamani hapo kwa hatua zaidi
Hukumu hiyo iliyomwamuru Babu Tale na nduguye kulipa kiasi
hicho cha fedha, ilitolewa na Jaji Agustine Shangwa, Februari
18,2016 katika kesi ya madai namba 185 ya mwaka 2013, iliyofunguliwa
na Sheikh Mbonde kutokana akiwalalamikia ndugu hao kutumia mahubiri yake
kibiashara bila ridhaa yake.
Babu Tale mbaroni kwa amri ya Mahakama
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 22, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 22, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment