Baada ya kukaa naye na kumtathimini
kwa takribani wiki mbili, hatimaye klabu ya Yanga imefikia makubaliano ya
imemsainisha mkataba kocha wake mpya Mwinyi Zaheri ambaye ni raia wa DR Congo.
Yanga ambayo imepokonywa ubingwa wa
ligi kuu na Simba SC, imekubaliana na mtaalam huy o wa ufundi kwa mkataba wa
miaka miwili ya kuifundisha Yanga ambayo inacheza makundi ya Kombe la
Shirikisho Afrika.
Zahera amechukua rasmi mikoba ya
Mzambia George Lwandamina aliyekuwa kocha mkuu wa kikosi cha Yanga baada ya
kuondoka kimyakimya kurejea kwao Zambia katika klabu yake ya zamani, Zesco
United.
Zahera ni kocha msaidizi wa timu ya
taifa ya DRC, The Leopard na mwenye uzoefu wa kufundisha soka katika bara la
Ulaya pamoja na Afrika.
Licha ya kusaini mkataba huo, Zahera
ameondoka nchini kwenda kwao Congo kwa majukumu ya kukitumikia kikosi cha timu
ya Taifa ya Congo na baadae atarejea nchini kuendelea na Yanga.
Yanga yachukua maamuzi haya
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 19, 2018
Rating:

No comments:
Post a Comment