Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa
nchi Kavu na Majini SUMATRA Mkoani Tabora imawaomba viongozi wa madhehebu
mbalimbali ya dini kuisadia serikali kuwaelimisha wananchi kuzingatia sheria za
usalama barabarani ili kuweza kupunguza ajali mkoani humo
Ombi hilo limetolewa na Afisa
mfawidhi wa mamlaka hiyo mkoani Tabora bwana Joseph Maiko wakati akizungumza na
East Radio Ofisini kwake.
Amesema viongozi wa dini wanakutana
na watu wengi katika nyumba zao za ibada hivyo ni vyema kuisaidia serikali
kuwaelimisha wananchi juu ya umuhimu wa kuzingatia sheria za usalama barabarani
ili kupunguza tatizo la ajali mkoani humo.
Aidha Bw. Maiko ameongeza kuwa
watumiaji wengi wa vyombo vya moto bado hawazingatii sheria za usalama
barabarani na hivyo kuwepo kwa ajali nyingi zisizotarajiwa mkoani humo.
Akizungumza kwa niaba ya viongozi wa
madhebu ya dini mkoani humo Shekhe Ramadhani Rashidi Juma amesema wao kama
viongozi wa dini wamepokea ombi hilo na kuahadi kushirikiana na serikali katika
kupunguza tatizo la ajali mkoani humo.
Viongozi wa dini waombwa kuisaidia sumatra
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 19, 2018
Rating:

No comments:
Post a Comment