Wenyeviti wa
jumuiya tatu za CCM wamekutana na kufanya mazungumzo na Rais John Magufuli ili
kuangalia namna ya kuziendesha jumuiya hizo kwa ufanisi
Viongozi hao
ni Edmund Mndolwa wa Jumuiya ya wazazi Tanzania, Gaudencia Kabaka wa
Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) na Kheri James mwenyekiti wa umoja wa
vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM).
Taarifa
iliyotolewa leo Mei 25 , 2018 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu,
Gerson Msigwa imesema viongozi hao wamekutana na Rais Magufuli kumueleza
maendeleo ya jumuiya zao sambamba na kumpa salama kutoka kwa Rais wa Afrika ya
Kusini Cyril Ramaphosa na rais wa Zimbambwe Emmerson Mnangagwa na
viongozi wa vyama tawala vya ANC cha Afrika Kusinji na Zanu-PF cha Zimbabwe
ambavyo vyama rafiki vya CCM
“Tumekuja
kumueleza ziara yetu ilikuaje lakini zaidi ya hapo, sisi wenyeviti wake wa
jumuiya tumekuja kuzungumza naye ili tuweze kuendesha jumuiya zetu kwa
ufanisi,”amesema Mndolwa.
Kabaka amesema:“Tumekuja
na salama kutoka kwa marais wa Afrika Kusini na Zimbabwe. Wanasema
wanatuheshimu sana na wanatutegemea, pia wametaka urafiki wa vyama vyetu
uendelee.”
Kwa upande wa
James, amesema wamefikisha salama za vijana wa CCM kwa vyama rafiki vya ANC na
ZANU-PF ambavyo vinatambua mchango mkubwa wa chama tawala katika kufikisha
mataifa yao kwenye mafanikio makubwa ya uhuru na maendeleo walionayo hivi sasa.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Rais Magufuli
alikutana na kufanya mazungumzo na Rais
mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa na makamu mwenyekiti
wa CCM, Philip Mangula.
Wenyeviti jumuiya za CCM wakutana na Rais Magufuli
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 25, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment