Tanesco inadai mabilioni, inadaiwa mabilioni


Waziri wa Nishati, Dk Merdad Kalemani amesema Shirika la Umeme Tanzani (Tanesco) linadaiwa Sh938 bilioni

Amesema Tanesco inakabiliwa na madeni hayo huku ikidai zaidi ya Sh200 bilioni

Waziri Kalemani amesema hayo bungeni leo Mei 25, alipokuwa akihitimisha hoja ya bajeti yake kwa mwaka 2018/19

“Kwa sasa tunafanya uhakiki wa madeni hayo ili kutoa mwelekeo wa nini kifanyike,” amesema

Amesema  Tanesco kwa sasa limeanza kuimarika kwa kiasi kikubwa na makusanyo ya mapato yake yameongezeka kutoka Sh 29 bilioni kwa wiki na kufikia 32.5 bilioni

“Lakini Tanzania ipo juu kwa usambazaji wa umeme vijiji ambao umefikia asilimia 49.5,” amesema
Tanesco inadai mabilioni, inadaiwa mabilioni Tanesco inadai mabilioni, inadaiwa mabilioni Reviewed by KUSAGANEWS on May 25, 2018 Rating: 5

No comments: