Wafanyabiashara
wa Mkoa wa Geita wamejitolea kuchangishana zaidi ya Sh4 bilioni
zitakazotumika katika ujenzi wa nyumba 100 za polisi mkoani humo
Mradi huo
unaotekelezwa katika eneo la makazi ya polisi Mtaa wa Magogo Kata ya Bombambili
mjini Geita ukikamilika utapunguza uhaba wa nyumba za kuishi wa askari hao.
Akizungumza
leo Ijumaa Mei 25, 2018 wakati wa uzinduzi wa mradi huo jana, mwenyekiti wa
kamati ya ujenzi, Chacha Wambura ambaye ni Mkurugeni wa Shule za Waja za mkoani
Geita amesema kila mfanyabiashara atajitolea kujenga nyumba kuanzia hatua ya
msingi, ukuta na kumalizia kulingana na uwezo wake
"Kujenga
ukuta (boma) hugharimu kati ya Sh15 milioni hadi Sh20 milioni ambapo hadi
kukamilika, nyumba moja itagharimu zaidi ya Sh40 milioni,” amesema
Amesema kila
askari polisi katika mradi huo ataombwa kuchangia kwa hiari angalau mifuko
miwili ya saruji.
Huu utakuwa ni
mradi wa pili nchini kutekelezwa na wafanyabiashara kwa hiari baada ya ule wa
mkoa wa Arusha ambapo wafanyabiashara walihamasishwa na kushiriki ujenzi wa
nyumba kwa ajili ya makazi ya askari polisi.
Wafanyabiashara wajitolea kuchangishana Sh4 bilioni kujenga nyumba 200 za polisi
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 25, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment