Ikiwa leo ni siku ya Afrika, lugha
za asili za Afrika nazo zimepigiwa chepuo ya kuwa chachu ya maendeleo na ukuaji
wa uchumi miongoni mwao ni lugha ya Kiswahili ambayo barani Afrika pekee
inaongoza kwa kuzungumzwa na watu wengi zaidi, huku idadi ikitajwa kuwa ni
zaidi ya watu milioni 200.
Akizungumzia nafasi ya lugha hiyo
katika kuchagiza maendeleo barani humo, Profesa Aldin Mutembei wa Taasisi ya
Taaluma za lugha ya Kiswahili ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam, TATAKI amesema
hilo linawezekana iwapo vijana watapatiwa fursa ya kusoma masomo ya sayansi na
teknolojia kwa lugha yao hiyo ya asili.
"Mpaka sasa tayari chuo kikuu
kimeshaandika vitabu kadhaa vya masomo ya sayansi kwa lugha ya kiswahili
ambavyo vinaweza kuingizwa katika mitaala ya elimu ya sekondari ili kutumika
kwa ajili ya kufundishia",amesema
Prof. Mutembei.
Aidha Prof. huyo ameongeza kuwa
ingawa baadhi ya waswahili wanapuuza matumizi ya lugha ya kishwahili katika
fani mbalimbali zinazohusu teknolojia lakini kuna baadhi ya nchi zimeanza
kupiga hatua katika ufundishaji wa lugha hiyo ambazo zinaelekea kuwa na
wabobezi wa lugha ya kiswahili.
Kiswahili chaongoza Africa
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 25, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment