Kijana mmoja nchini Uganda
ameshitaki kanisa moja nchini humo akipinga kanuni za utaratibu wa kufunga ndoa
akieleza kuwa zinakwenda kinyume na katiba.
Kijana Michael Aboneka amepeleka
kesi hiyo katika mahakama ya katiba mjini Kampala kulishtaki kanisa la Watoto
Church kwa madai kuwa linawanyima vijana wengi haki yao ya kikatiba ya kufunga
ndoa na wapenzi wao baada ya kutimiza umri wa miaka 18 kama katiba ya Uganda
inavyosema.
"Kwanza wanasema nilazima
upate barua kutoka kwa wazazi wa bibi harusi ambayo wanaita Baraka. Kwangu
inakwenda na kinyume cha katiba kifungu 31 ya ndoa ya pili ni kukabidhi barua
ya Daktari ya majibu ya kupima virusi vya ukimwi kwa kanisa"
Aboneka.
Ameongeza kuwa "Nimekwenda
hospitalini kupimwa na mchumba wangu tumepata majibu tunafahamu majibu ya kila
mmoja wetu. Kwa hiyo mimi na mchumba wangu kukabidhi vipimo vya ukimwi kwa
kanisa inavunja haki ya uhuru wa siri zetu, nimekuta ni kinyume na katiba'.
amesema Aboneka.
Aboneka ameongeza kusema kuwa siyo
kanisa la Watoto pekee lenye utaratibu huo bali makanisa mengi nchini yanafanya
hivyo na anasema ameiomba mahakama ya katiba kuanza mara moja kusimamisha
kanuni hizo na anatarajia wiki hii mahakama inaweza kutoa jibu.
Aboneka amesema kuwa siyo kwamba ana
chuki na kanisa la watoto, ila ni kusaidia vijana wengi ambao wameshindwa
kufunga ndoa zao ili mahakama ya katibu itowe ufumbuzi wa swala hilo.
Alishtaki kanisa kwa kuvunja katiba
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 25, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment