Jeshi la
Polisi linakabiliwa na ukinzani mkali dhidi ya pendekezo la kutaka kuwaruhusu
maofisa wake kuwashikilia watuhumiwa wa uhalifu kwa zaidi ya siku mbili kabla
ya kupewa dhamana au kufikishwa mahakamani
Wakati polisi
wanasema mabadiliko hayo yatawahusu watuhumiwa wanaohusishwa na ugaidi,
wapinzani wanadai kwamba upo uwezekano hata watuhumiwa wa makossa madogo pia
kushikiliwa kwa muda mrefu.
Polisi wanasema baadhi ya makosa, kama vile
ugaidi, yanahitaji uchunguzi kupata ushahidi na mashahidi kutoka nje ya mipaka.
Mamlaka hiyo inahitaji kuungwa mkono na Bunge kwa kubadili Ibara ya 23 ya
Katiba ili polisi waweze kuwashikilia watuhumiwa wa ugaidi kwa siku kati ya
saba na 14 kabla ya kufikishwa kortini
Naibu msemaji
wa Jeshi la Polisi, Patrick Onyango alisema wakati mwingine kuhakiki sampuli
zilizopatikana katika maeneo ya uhalifu kunahitaji muda wa kutosha kwa sababu
“sisi pia tunatumia uhakiki wa maabara za serikali nyingine. Pia wanahitaji
muda.”
"Wakati
mwingine wanasema, 'tumeshtushwa na sampuli ... hizi sampuli
mnazotuletea,'" aliongeza. "Kwa hiyo tunawaomba wabunge, kwamba
katika baadhi ya matukio wanapaswa kubadili katiba ili waturuhusu tuweze kukaa
na watuhumiwa kwa walau zaidi ya saa 48."
Kabla ya
pendekezo hilo kusonga mbele lazima liungwe mkono na Kamati ya Kudumu ya Bunge
ya Haki za Binadamu. Mwenyekiti wa kamati hiyo Jova Kamateka ameonyesha shaka.
Anasema wamevurunda sheria.
Polisi Uganda wataka kushikilia
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 25, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment