Waziri wa Nishati asema mbio zimeanza rasmi

Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani amesema mbio za kutatua kero za wananchi kuhusu matumizi mbalimbali ya nishati ikiwamo ya kupikia sasa zimeanza rasmi

Dk Medard ambaye pia ni Mbunge wa Chato ametoa kauli hiyo leo, Jumapili Mei 20, 2018, wakati akizindua ujenzi wa miundombinu ya kuunganisha bomba la gesi asilia kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam

Uzinduzi huo ulifanyika Ubungo jijini hapa na unatarajia kukamilika Septemba mwaka huu.

Kadhalika bomba hilo la gesi litawaunganisha wananchi 1,000 wa mikoa ya Dar es Salaam na Mtwara watakaonufaika na gesi hiyo

“Leo nazindua, lakini kazi kubwa ni utekelezaji na kuwafikishia miundombinu Watanzania ili wapate manufaa ya matumizi ya rasilimali hii ya gesi,” amesema Dk Kalemani

Amesema ujenzi wa miundombinu hiyo utagharimu Sh 4bilioni kwa awamu ya kwanza na maeneo yatakayonufaika ni Mikocheni, Ubungo, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Sinza, Shekilango na Makongo Juu

Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Mhandisi Kapuulya Musomba amesema hivi sasa wanafanya usanifu ili kujua watu wangapi watapata huduma ya gesi kwa upande wa Dar es Salaam



Waziri wa Nishati asema mbio zimeanza rasmi Waziri wa Nishati asema mbio zimeanza rasmi Reviewed by KUSAGANEWS on May 20, 2018 Rating: 5

No comments: