|
Pamoja na Mkoa wa Mbeya kuwa na
idadi kubwa ya wagonjwa wanaoishi na Virusi vya Ukimwi, Bohari ya Dawa
(MSD), imesema itahakikisha hakuna anayekosa dawa za kufubaza makali ya
Virusi vya Ukimwi(ARV's
Mkoa huo ni wa tatu kwa maambukizi
kitaifa ukiongozwa na Njombe unaoshika nafasi ya kwanza na Iringa nafasi ya
pili
Akizungumza na waandishi waliopo
ziarani mkoani humo, Meneja Kanda ya Mbeya wa Bohari hiyo, Benjamin Hubila,
amesema hadi sasa hali ya upatikanaji wa dawa hizo katika vituo
wanavyovihudumia ipo vizuri
Waandishi hao wapo katika ziara ya
kujionea utekelezaji wa mpango wa usambazaji wa dawa wa moja kwa moja katika
vituo unaofanywa na MSD
Hubila amesema ingawa kuna uhitaji
mkubwa wa dawa hizo ukilinganisha na maeneo mengine wanayoyahudumia,
wanahakikisha dawa hizo zinapatikana wakati wote
“Upatikanaji wa dawa katika maeneo
wanayohudumia ikiwemo Rukwa, wilaya ya Makete na Mbeya ni wa asilimia 95 hadi
100,” amesema.
Hubila alizungumzia wizi wa dawa
na kusema wanashirikiana na kamati za ulinzi za mkoa na wilaya kufuatilia
suala hilo
"Nadhani suala la wizi wa
dawa za serikali pia limepungua kutokana na kuwekwa nembo ambayo ni rahisi
kumtambua mtu anayeiiba," amesema meneja huyo.
|
|
MSD yasema hakuna mgonjwa atakayekosa ARV's
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 20, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 20, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment