Siku 11 baada ya mbunge wa Mbeya, (Chadema)
Joseph Mbilinyi maarufu ‘Sugu’ kuachiwa huru, kesho Mei 21, 2018 ataingia
bungeni
Sugu ataingia bungeni kuwawakilisha wananchi
wa Mbeya baada ya kulikosa bunge hilo la bajeti tangu lilipoanza Aprili mwaka
huu
Akizungumza Sugu amesema: “Nipo Dodoma
tayari, nimekuja baada ya hali ya mama yangu kuendelea kuimarika na kesho (Mei
21,2018) nitaanza kuwawakilisha wana Mbeya walionituma.”
“Wana Mbeya walikosa mwakilishi, walikosa wa
kuwasemea mambo yao, kwani kilichotokea juu yangu ilikuwa kuwanyima fursa Mbeya
kusikika ndani ya mjengo, sasa nimerudi kuwatumikia kwa nguvu zangu zote.”
Amesema kile kilichomtokea kimemwongezea
umaarufu zaidi ya aliokuwa nao, “unajua mimi nilikuwa maarufu lakini kwa hiki
kilichonitokea, nimekuwa mashuhuri na si maarufu tena.”
“Nikiwa njiani, Makambako wananchi wamenipa
pole na wengine pongezi, sawa na Iringa na hapa Dodoma na kila mahali
ninapopita, watu wanapiga picha na mimi, sasa utasema ni maarufu, mimi ni
mashuhuri,” ameongeza:
Sugu na Katibu wa Chadema, Kanda ya Nyasa,
Emmanuel Masonga walihukumiwa Februari 26, 2018 kwenda jela miezi mitano na Mahakama
ya Hakimu Mkazi, Mbeya baada ya kuwakuta na hatia ya kutoa lugha ya fedheha
dhidi ya Rais John Magufuli
Mei 10, Sugu na Masonga waliachiwa huru kwa
msamaha wa Rais Magufuli alioutoa Aprili 26, 2018 wakati wa sherehe za Muungano
Sugu kutinga bungeni kesho
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 20, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 20, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment