Mbunge wa Mchinga (CUF), Hamidu Bobali
amesema Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango ni miongoni mwa
mawaziri waliofeli kwa kukwamisha miradi mbalimbali inayotekelezwa na
Serikali
Bobali ametoa kauli hiyo leo Mei 24, 2018
katika mjadala wa bajeti ya Wizara ya Nishati mwaka 2018/19
Amesema miradi ya umeme vijijini na
mingineyo inakwama kwa kuwa waziri huyo hatoi fedha licha ya Waziri wa Nishati,
Dk Medard Kalemani kuzindua miradi mbalimbali ya Wakala wa Umeme Vijijini (Rea
“Kama Dk Mpango ataendelea kuwa waziri kwa
miaka mitano atakwamisha miradi mingi na kama kuna waziri aliyefeli zaidi
ni Mpango. Wizara ya Kilimo, Maji, Tamisemi zimelia hazina fedha, “ amesema
Bobali amemtaka Dk Kalemani atakapokuwa
akihitimisha hoja yake kueleza utekelezaji wa mpango wa umeme wa Power Afrika
uliozinduliwa mwaka 2013 na aliyekuwa Rais wa Marekani, Barack Obama
“Waziri ukija utueleze Power Africa imefikia
wapi kuna taarifa Power Africa iliondoka baada ya Rais Kikwete (Jakaya-rais wa
Awamu ya Nne) kuondoka madarakani,” amesema
Kwa upande wake mbunge wa Ukonga (Chadema),
Mwita Waitara amesema wabunge wanamsubiri Dk Mpango atakapowasilisha bajeti
yake bungeni kutokana na wizara yake kushindwa kutoa fedha z amiradi ya
maendeleo
“Dk Mpango watu wanakusubiri utuambie kama
fedha hakuna tupange namna ya kupata fedha. Ili watu watoke gizani na wasitumie
mkaa ni lazima umeme na gesi uuzwe kwa bei nafuu. Ukonga tu pale hakuna umeme,
mimi pale nina mitaa tisa haina umeme, mingine miwili ya kata ya Msongola
hakuna umeme, Chanika, Buyuni nako hakuna umeme,”amesema.
Waziri wa Fedha atajwa kukwamisha miradi ya maendeleo
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 24, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment