Mbunge wa Vunjo (NCCR-Mageuzi), James Mbatia
ametoa mapendekezo manne akitaka yafanyiwe kazi na Serikali ili kuwalinda
wananchi na madhara yanayosababishwa na mvua
Akitoa maelezo binafsi bungeni leo Mei
24,2018 Mbatia amesema mvua zinazonyesha nchini zinaharibu miundombinu na
kuwaacha wananchi bila makazi
Amesema Serikali imeshindwa kutimiza wajibu
wake wa kuwakinga, kuwalinda na kuwaokoa raia wake dhidi ya majanga
Akiyataja mambo hayo manne amesema,
"Kwanza Serikali ijitahidi kulinda uhai huo hasa huduma muhimu za kukuza
utu wao mfano huduma za chakula, maji safi na salama, afya, makazi na nyinginezo."
Amesema jambo la pili ni Serikali kuboresha
miundombinu ya shule za msingi na sekondari
“Tatu Serikali irudishe miundombinu ya
mawasiliano hususani ya barabara zitakazopitika muda wote,” amesema
“Jambo la nne ni Serikali kuanzisha wakala
wa usimamizi wa majanga kama inavyotakiwa na sheria ili ifanye jukumu moja la
kuwakinga, kuwalinda na kuwaokoa raia wake dhidi ya majanga ya aina
mbalimbali,” amesema.
Mbatia aeleza mambo manne ya kujikinga na madhara ya mvua
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 24, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment