Waziri wa habari sanaa
michezo na utamaduni Dokta Harson Mwakyembe amewataka watanzania kutumia
fursa zilizopo kwa kufanya kazi kwa bidii na kwa maarifa ili kuweza kujiingizia
kipato na kuongeza pato la taifa na
hatiye kufikia uchumi wa kati.
Dokta mwakyembe ametoa rai hiyo wakati akifungua
jukwaa la fursa za biashara Mkoani Arusha ambapo amesema kuwa pamoja na
changamoto zilizopo ni vema watanzania wakafanya kazi kwa biidii kwa kugeuza
changamoto hizo kuwa fursa kwani wasipotumia fursa hizo ipasavyo watu wengine
kutoka nje wataziona kuzichangamkia.
Ameeleza jukwaa hilo ni mahususi kwa ajili ya
kuhamasisha hari kwa kuchangamsha shughuli za kiuchumi Mkoani hapa ili kuufanya
kuwa namba Moja katika kuvutia wawekezaji ikiwa ni pamoja na kuhamasisha
wananchi na wageni kutumia fursa zilizopo ambapo iwapo jukwaa hilo litatumika
vizuri litaweza kuvutia wawekezaji wengi zaidi ndani na nje ya nchi
Dokta Jim Yonazi Mhariri mtendaji wa kampuni ya magazeti
ya serikali (TSN) ambapo ni waandaji jukwaa hilo amesema kuwa wameiangalia
Tanzania kama nchi inayopiga kazi ya maendeleo hivyo wanahamasisha kwa
kushiriki kwa vitendo ili kuweza kuibua fursa na kuzipeleka kwa wadaukupitia jukwaa
hilo ili nchi iweze kuendelea na kufikia uchumi wa kati.
Kwa upande wake Moses Mabula mchumi Mkuu wa ofisi ya
Mkoa wa Arusha amesema kuwa pato la Mkoa limepanda kutoka trilioni 2.3 hadi trillion 4.2 na
imefanikisha kuwa ya 7 kwa uchangiaji wa pato la taifa na kuwa ya 3 kwa
ongezeko la pato la mkazi kutoka billion 1.2 hadi kufikia billion 2.3.
Naye Ester Ally Mtwalizya ameeleza kuwa jukwaa hilo
litasaidia wajasiriamali kutangaza bidhaa zao ndani na nje ya Mkoa ikiwa ni
pamoja na kubadilishana uzoefu hali itayofanya wasonge mbele.
MWAKYEMBE;TUSIPOTUMIA FURSA ZETU NCHINI WATU KUTOKA NJE WATAZIONA NA KUZICHANGAMKIA
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 24, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment