Chama
cha Wananchi (CUF), kimesema kimeandika barua rasmi kwa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli ili kusaka muafaka wa kisiasa Visiwani
Zanzibar.
Kauli hiyo ya CUF imetolewa leo Jijini Mwanza na
Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharrif Hamad katika mahojiano maalum
yaliyoratibiwa na Umoja wa Vilabu Vya Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) na
kurushwa na vituo mbalimbali vya redio na mitandao ya kijamii.
"Mpaka sasa Ikulu bado
haijajibu barua hiyo. Licha ya kuwepo kwa miafaka zaidi ya minne kati ya CUF na
Chama cha Mapinduzi (CCM), lakini kumekuwa hakuna utashi wa kisiasa katika
kusaka muafaka wa moja kwa moja kuhusu tofauti za kisiasa huko Zanzibar", amesema
Maalim Seif.
Maalim Seif amewahi kuhudumu katika nyadhifa
mbalimbali Visiwani Zanzibar, ikiwemo ya Waziri wa Elimu kwenye serikali ya
Hayati Mzee Aboud Jumbe, Waziri Kiiongozi kwenye serikali ya Mzee Ali Hassan
Mwinyi na Makamu wa Kwanza wa Rais kwenye serikali ya Dkt. Ali Mohamed Shein
awamu ya kwanza baada ya kufikiwa kwa makubaliano ya kuundwa serikali ya Umoja
wa Kitaifa mnamo mwaka 2010.
CUF yaomba suluhu kwa Rais Magufuli
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 24, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment