Waziri wa Viwanda,
Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage amewataka wanafamilia, wafanyakazi na
watanzania kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kigumu ambapo Taifa limepoteza
maofisa watatu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).
Waziri Mwijage amesema hayo leo Mei
24, 2018 katika ibada ya kuaga miili ya waliokuwa wafanyakazi watatu wa kituo
cha uwekezaji waliofariki katika ajali ya gari eneo la Msoga na kuongeza kuwa
anatambua wakati mgumu wanaopitia familia ya watumishi hao kwa kupoteza
wapendwa wao kwasababu hata yeye alimpoteza mama yake akiwa na miaka sita.
“Hakuna zaidi ninaloweza kufanya,
familia ni muhimili, uzoefu wangu mbaya hauwezi kuwa nafuu kwenu lakini hawa
watoto wadogo wanaweza kufanana na mimi, nilimpoteza mama yangu nikiwa nina
miaka sita lakini haya ni mapenzi ya Mungu” amesema Mwijage.
Waziri Mwijage ameongeza kuwa, Taifa
limepoteza watu muhimu katika jitihada za kukuza sekta ya uwekezaji nchini na
kuwataka wafanyakazi wengine wa kituo hicho kutohuzunika sana bali wawakumbuke
wenzao kwa kufanyakazi kwa bidii.
Mei 21, 2018 katika eneo la Msoga
mkoani Pwani watumishi watatu wa Kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC) walifariki
Dunia baada ya gari waliyopanda kugongana na lori walipokuwa wakisafiri kikazi
kuelekea Dodoma, waliofariki ni Martin Laurence (39), Zakaria Nalinga (49) na
Said Moshi.
“Nilimpoteza mama nikiwa na miaka sita”- Mwijage
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 24, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment