Mamlaka ya Mapato nchini
TRA imesema mahusiano na ushirikiano kati
ya mamlaka na wafanyabiashara umeendelea
kuimarika na kuleta tija kwa wananchi na
taifa kwa hatua ambayo mkurugenzi wa elimu
ya mlipakodi Bw. Richard Kayombo amesema umeanza
kurahisisha ulipaji wa Kodi na pia
kupunguza gharama za ukusanyaji.
Akizungumza na walipakodi mkoani Arusha
Bw. Kayombo amesema baada ya
wafanyabishara kuanza kuelewa umuhimu wa
kulipa kodi na pia kuona matokeo ya
kodi zao asilimia kubwa sasa wanalipa
kwa hiyari na wanatoa ushirikiano mkubwa ukiwemo
wa kufichua wachache wanaoendelea kukwepa kodi
na mbinu wanazotumia
Kuhusu hatua iliyofikiwa kudhibiti
ukwepaji wa kodi kwa bidhaa zinazotoka nje
Bw. Kayombo amesema pia tatizo hilo
linaendelea kupungua kutokana na kuimarishwa
kwa ushirikiano na wenzao wa nchi jirani na
ameendelea kuwaomba wafanyabishara kutumia fursa
za soko la pamoja na Jumuiya ya Afrika
Mashariki kufanya biashara halali ili kuepukana
na hasara zisizo za lazima kwani
biashara za magendo kwa sasa hazina nafasi
Baadhi ya wafanyabishara wamekiri kuboreka
kwa mahusiano miongoni mwao na TRA na
wameitaka mamlaka hiyo kuendelea kuyaboresha
hasa wakati huu ambao hali ni ngumu
kwani hata wao wanafurahia kulipa kodi
na wanaona matokeo yake
Ushirikiano wa TRA na wafanyabiashara waendelea kuimarika
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 24, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment