TRA Kilimanjaro yateketeza bidhaa zilizoingizwa nchini kinyemela


Mamlaka ya mapato nchini  (TRA)mkoani Kilimanjaro imeteketeza shehena ya bidhaa mbalimbali  za vyakula yakiwemo mafuta ya kupikia ,vifaa vya hospitali ,na vipodozi vyenye viambata vya sumu vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 23 ambavyo vimeingizwa nchini  kupitia njia za panya.

Meneja msaidizi wa Forodha mkoa wa Kilimanjaro Bw.Godfrey Kitundu amesema wafanyabiashara wenye bidhaa hizo walikwepa kulipa kodi  na nyingine zimeisha muda wake wa matumizi kwa ajili ya binadamu

Bidhaa zilizokamatwa ni mafuta ya kupikia,mifuko ya chumvi ya kupikia,vipodozi aina mbalimbali,vifaa tiba,chemikali za hospitali zilizoisha muda wake ambazo ni hatari kwa watumiaji pamoja na vitabu vya dini ambavyo havijateketezwa ili kupata utaratibu wa vitabu hivyo

Kwa upande wake mkaguzi wa mamlaka ya chakula na dawa Tanzania (TFDA) mpaka wa Holili Bw.Edward Mwamilao amesema  bidhaa  zilizoteketezwa ni hatari kwa afya za binadamu endapo zingeingia sokoni

Nao baadhi wa wananchi wamepongeza hatua iliyochukuliwa kuteketeza  bidhaa hizo ambazo zimekuwa zikileta madhara makubwa kwa wananchi.



TRA Kilimanjaro yateketeza bidhaa zilizoingizwa nchini kinyemela TRA Kilimanjaro yateketeza bidhaa zilizoingizwa nchini kinyemela Reviewed by KUSAGANEWS on May 24, 2018 Rating: 5

No comments: