Waziri wa zamani wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Charles Kitwanga amesema kama Waziri wa Fedha, Dk Philip Mpango anadai
hana fedha za kutekeleza miradi mbalimbali ni vyema akajiondoa katika wadhifa
huo.
Kitwanga ambaye ni mbunge wa Misungwi (CCM)
ametoa kauli hiyo leo jioni Alhamisi Mei 24, 2018 katika mjadala wa bajeti ya
Wizara ya Nishati mwaka 2018/19
Mbunge huyo ameishauri Serikali kuangalia
mipango ya kuanzisha miradi mikubwa ya kuzalisha umeme, kuachana na miradi
midogo
“Hivi kwanini unakosa fedha? Kama ni waziri
wa fedha halafu unasema hakuna fedha ondoka hapo,” amesema.
Amesema miradi midogo ina gharama kubwa za
uendeshaji ikiwemo kuwalipa mishahara watumishi wanaohudumia katika vituo hivyo
na kumshauri Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani kuja na mpango
wa kuzalisha umeme wa Megawati 5,000 kwa kutumia makaa ya mawe
“Wazungu wanasema uzalishaji wa umeme kwa
kutumia makaa ya mawe unachafua hali ya hewa lakini wao wanazalisha umeme kwa
kutumia makaa hayo kwa sababu teknolojia imebadilika,” amesema
“Duniani kote umeme wa bei nafuu ni
unaozalishwa na maji ama Makaa.”
Kitwanga amtaka Dk Mpango kung’oka
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 24, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment