Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema upimaji wa
Kifua Kikuu (TB) na Ukimwi kwenye baa hautakuwa wa lazima.
Akizungumza wakati wa
maadhimisho wa miaka 30 ya Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Ukimwi (NACP), Mwalimu alisema
baada ya kutolewa taarifa ya kuwapo mpango huo watu wengi wamekuwa na
hofu.
“Tutatekeleza mpango
wa kusogeza huduma za upimaji TB na ukimwi kwenye baa, ila hautakuwa wa lazima,
tutachofanya ni kuwashawishi wananchi kutumia fursa ya kusogezewa huduma
hiyo,”alisema.
Aidha, alisema kwa
sasa wizara yake iko katika mkakati wa kufanyia marekebisho ya Sheria ya Ukimwi
kwa lengo la kuruhusu watu kujipima mwenyewe, kutoa fursa kwa vijana kuanzia
miaka 15 kwenda kupima ukimwi bila kupata ridhaa ya wazazi au walezi.
“Haya ni maeneo ambayo
kama tutayafanyia marekebisho tutaweza kusaidia kuongeza kasi ya kudhibiti
maambukizi ya Ukimwi,” alisema.
Katika hatua nyingine,
Mwalimu aliagiza kuanzia Julai mosi mwaka huu, watu wanaoishi wa virusi vya
Ukimwi kupewa dawa za miezi mitatu badala ya sasa ya kupewa kwa miezi
mwili.
Agizo alilitoa
kutokana na Mwenyekiti wa Baraza la Watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi, Justin
Mwinuka kudai kuwa utaratibu wa kupewa dawa za miezi miwili umekuwa ukiongezea
gharama, kwani wamekuwa wakitakiwa kupima afya zao kila baada ya miezi
mitatu.
Waziri huyo alisema
utaratibu huo wa kuwapa dawa kwa miezi mitatu mitatu uanze haraka isipokuwa kwa
wale ambao wanaonekana hawataweza kutunza dawa hizo au ambao ndio kwanza
wanaanza kutumia dawa hizo.
Waziri wa Afya: Upimaji UKIMWI baa sio lazima
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 13, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 13, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment