Warembo wawili ambao
walifahamika kwa majina ya Ashura na Zubeda, wamedaiwa kuzichapa kavukavu
chanzo kikitajwa kuwa ni kumgombea baba wa msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul
‘Diamond Platnumz’, Abdul Juma.
Tukio hilo
lililokusanya watu lilitokea hivi karibuni katika baa moja maarufu kwa jina la
Suma iliyopo maeneo ya Magomeni-Kagera jijini Dar ambayo baba wa msanii huyo
anadaiwa kuwa anakwenda mara kwa mara kupata ‘kinywaji’.
Taarifa zaidi
zinaarifu kuwa, warembo hao walitangulia kufika katika baa hiyo na kupiga stori
pamoja huku wakipata kilevi lakini baadaye alipotokea baba Diamond na kujumuika
nao, kila mmoja alianza kujitapa kuwa ni wake.
“Yani walianza
kubishana. Ghafla wakaanza kushikana na ndipo watu walipowawahi na kuwaamua.
Baba Diamond kukwepa soo akaamua kutoweka eneo hilo,” kilidai chanzo
Baba Diamond Agombaniwa na Warembo Kirabuni
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 13, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 13, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment