Katika kukabiliana na
tatizo la Ujangili nchini, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi
Kigwangalla, amekabidhi magari 6 kwa Halmashauri sita tofauti yatakayotumika
kwa ajili ya kupambana na vita hiyo.
Kwa niaba ya Halmashauri hizo,
Kigwangalla amewakabidhi magari hayo Wabunge kwenye ofisi za Makao Makuu ya
Wizara ya Maliasili na Utalii Jijini Dodoma.
Wabunge waliokabidhiwa magari hayo
ni wa Bunda Vijijini Boniface Getere, Mbunge wa Itilima Njalu Silanga,
mbunge wa Longido Dk. Steven Kiruswa, Mbunge wa Mbulu Vijijini Flatei Massay na
Mbunge wa Tanganyika Moshi Kakoso.
Kwa upande wake Mbunge wa
Ngorongoro, William Ole Nasha hakuweza kufika kutokana na kubanwa na majukumu
mengine katika Wizara yake ya Elimu lakini atakabidhiwa atakapofika ofisini
hapo.
Waziri Kigwangalla amesema
wamekabidhi magari hayo kwa wilaya hizo kwa kuzingatia sifa na mahitaji
kwasababu zipo pembezoni mwa hifadhi mbalimali za taifa hivyo uwepo wa magari
hayo utarahisisha zoezi hilo.
Kigwangalla atoa magari kwa Wabunge 6
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 13, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 13, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment