Chama cha ACT Wazalendo
kimeitaka Serikali kuwaruhusu wanafunzi wa vyuo vikuu wafanye siasa vyuoni kwa
taratibu zilizowekwa kwa sababu vyuo ni kitovu cha mabadiliko ya jamii ikiwa ni
pamoja na kuwa chimbuko la viongozi mbalimbali.
Wito huo umetolewa leo na Katibu wa
Itikadi, Mawasiliano na Uenezi wa chama hicho, Ado Shaibu ambapo amekinzana na
kauli ya Rais Magufuli aliyoitoa siku chache alipotembelea Chuo cha
Kilimo cha Sokoine kuwataka wanafunzi wasifanye siasa vyuoni.
Kiongozi huyo amesema "Kupiga
marufuku siasa vyuoni ni kujenga taifa la vijana waoga, wasiokuwa na uwezo wa
kuhoji. Vijana msiache kuhoji mambo ya msingi kwa jamii zenu, hiyo ndiyo
maana ya usomi" na kwamba maisha ya siasa wakiwa vyuoni ndiyo
yaliwapa ujasiri wa kuingia kwenye ulingo wa siasa.
Mbali na hayo Chama hicho kimeshauri
kuwepo kwa mfumo mpya wa utoaji mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu, kutokana
na mfumo uliopo sasa kutokidhi mahitaji ya wanafunzi hali inayopelekea wengi
wao kukosa mikopo.
ACT wapingana na Magufuli
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 13, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 13, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment