Watu waliojitoa mhanga
wamevamia makanisa matatu nchini Indonsia na kuyalipua kwa mabomu.
Milipuko hiyo imetokea katika mji wa
pili kwa ukubwa nchini humo wa Surabaya na kusababisha vifo vya watu 9, huku
idadi hiyo ikitazamiwa kuongezeka.
Zaidi ya watu 13 wamepata majeraha,
baadhi yao mabaya sana. Misururu ya milipuko hiyo ya mabomu yalifuatana.
Hakuna kundi lolote lilokiri kuhusika
katika mashambulio hayo, lakini kundi linalojiita Jemaah Ansharut Daulah (JAD),
ambalo lina uhusiano na kundi la wapiganaji wa kigaidi wa Islamic State, huenda
lilihusika kwa mujibu ya Jeshi la polisi nchini humo.
Makanisa yavamiwa na kushambuliwa kwa mabomu
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 13, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 13, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment