Serikali yaweka wazi kuhusu upungufu wa sukari


Waziri  wa Kilimo Mhe. Dkt. Charles Tizeba, amefunguka kuwa hakutarajiwi kuwa na upungufu wa sukari hapa nchini kwa sababu hadi kufikia tarehe 10 mei 2018 katika maghala ya wazalishaji na wafanyabiashara  kulikuwa na tani 78,147.67 za sukari na kiasi kingine  tani 25,441.25 zipo Bandarini.

Waziri Tizeba amesema Serikali imeagiza sukari kiasi cha tani 70,354.35 kutoka nchi za nje lengo likiwa ni kujipanga ili kuhakikisha kuwa hapatokei upungufu wa bidhaa hiyo hapa nchini.

Waziri Tizeba amefafanua  kuwa tani 60,539.35 ya sukari  itaanza kuingia hapa nchini katikati ya mwezi Mei 2018 ambapo kiasi kilichobaki cha tani 9,815 kitaingia mwezi  June mwaka

"Kwa kiasi cha sukari  ambacho tayari kipo hapa nchini kikijumlishwa na kiasi ambacho kitaingia hivi karibuni kutoka nje ya nchi ni dhahiri kwamba  nchi haiwezi kupata upungufu wa bidhaa hiyo", alisema Mhe.Waziri.

Awali Dkt.Tizeba  alisema kwamba mahitaji ya sukari nchi nzima ni tani 630,000 ambapo kati ya hizo, tani 145,000 ni kwa ajili ya matumizi ya  viwandani na tani 485,000 ni kwajili ya matumizi ya kawaida.

Serikali yaweka wazi kuhusu upungufu wa sukari Serikali yaweka wazi kuhusu upungufu wa sukari    Reviewed by KUSAGANEWS on May 13, 2018 Rating: 5

No comments: