|
Ngombe 12 wanaosadikiwa kufa
wamekutwa wakichinjwa ndani ya lori eneo la mtaa wa Wazo kwa ajili ya
kusambazwa kwenye mabucha ya ngo’mbe
Akizungumza mmoja wa
mashuhuda Issa Ibrahim amesema wakati anaelekea msikitini saa 10
alfajiri aliliona gari aina ya lori limesimama pembezoni mwa barabara na
alipolisogelea aliwaona watu wakiwachuna ng’ombe waliokufa
Amesema aliwahoji na kuwakataza
wasiendelee kuwachuna ngombe hao kwa kuwa dini hairuhusu kula vibudu lakini
watu hao walikaidi na kuendelea kazi yao
“Wale watu walikuwa wengi kila
mmoja alikuwa na kisu chake huku wakichuna ngombe hao, kwa kuhofia usalama
wangu nilipiga simu msikitini ndipo walikuja eneo hili ili tuungane tuweze
kuwakamata lakini wote walikimbia na kuacha nyama zao kwenye gari,” amesema
Ibrahim
Katibu wa Kamati ya Afya na
Mazingira mtaa huo, Ally Kitokos amesema matukio ya kuchinjwa ng’ombe
waliokufa hujitokeza mara kwa mara na ndiyo maana hivi karibuni mmiliki
wa machinjio ya Wazo alimfukuza kazi mchinjaji mkuu baada ya kupingana na
kitendo cha kuchinja ngombe waliokufa
“Leo hii tunaona ng’ombe 12
wamekufa kibudu na wanaendelea kuwachuna kwa ajili ya kupelekwa kwenye
mabucha, wakati mchinjaji mkuu wa mwanzo alifukuzwa kwa kosa hilo,” amesema
|
Dili la kuingiza vibudu buchani lafichuka
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 13, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 13, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment