Mkazi wa Miembeni mjini Unguja, aliyetajwa kwa jina moja la Hassan
amenusurika kifo baada ya kutolewa ndani ya kontena alikojifungia
Msimamizi wa makontena katika Bandari ya Malindi, Ibrahim Abdallah
akizungumza amesema chanzo cha mtu huyo
anayekadiriwa kuwa na miaka 30 kuingia kwenye kontena na kujifungia
hakijajulikana
Amesema wakiwa katika kazi zao eneo hilo saa moja asubuhi
walisikia sauti ikitoka ndani ya kontena lililo juu ya jingine hivyo kuzua
taharuki miongoni mwao
Abdallah amesema sauti iliyosikika kutoka ndani ya kontena
ilisema, “Nakufaaa.”
Amesema walipofika eneo hilo waliuliza, “wewe ni nani” na jibu
walilopatiwa ni, “Hassan.”
"Baada ya kutaja jina tulifungua kontena ambalo alikuwa
amelifunga na kumtoa akiwa na hali mbaya kiafya na tulimpeleka Hospitali ya
Mnazi Mmoja ili kupatiwa huduma ya kwanza," amesema
Kuli katika bandari hiyo, Mohamed Khamis Makame amesema ni mara ya kwanza kutokea tukio hilo eneo hilo, hivyo amesema wanapaswa kuwa makini katika ulinzi
Sauti ndani ya kontena yazua taharuki bandarini
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 13, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 13, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment