|
Timu ya taifa ya
vijana chini ya miaka 20, imekubali kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa timu ya
vijana ya Mali kwenye mchezo uliomalizika jioni kwenye uwanja wa taifa jijini
Dar es Salaam.
Ngorongoro imejiweka kwenye
mazingira magumu ya kufuzu hatua inayofuata ikiwa na kazi ya kubadili matokeo
ugenini ili iweze kushinda na kufuzu kutokana na kuruhusu mabao ya ugenini
kwa Mali.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na
waamuzi kutoka Comoro, Soulaimane Ansudane aliyepuliza kipyenga akisaidiwa na
washika vibendera Mmadi Faissoil na Abdoulmadjid Azilani, hadi mapumziko
tayari Mali walikuwa mbele kwa mabao 2-1.
Ousmane Diakite alianza kuifungia
Mali bao la kuongoza kabla ya Samadiare Dianka kufunga bao la pili wote
wakitumia makosa ya walinzi na mlinda mlango Abdultwali Msheri.
Mshambuliaji chipukizi wa Azam FC,
Paul Peter ndiye aliyeifungia Ngorongoro Heroes bao la kufutia machozi dakika
ya 44 akiuwahi mpira uliotemwa na kipa wa Mali, Youssouf Keita kufuatia shuri
la mpira wa adhabu.
|
|
Tanzania yakubali kipigo cha Goli 2
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 13, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 13, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment