Mvua bado ipo ipo sana


Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA) imetoa tahadhari ya kunyesha mvua kubwa kwa siku tano kuanzia leo, ambazo zinaweza kuleta mafuriko katika maeneo ya mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani, Lindi, Mtwara na Visiwa vya Unguja na Pemba

Katika taarifa ya TMA iliyotolewa leo Mei 13, mvua hizo zilizoanza kunyesha leo, zitaendelea mpaka Mei 17 mwaka huu

TMA imesema athari zinazinaweza kutokea ikiwemo mafuriko ambayo yanaweza kusababisha kuvurugika kwa usafiri, barabara kubwa kutopitika na maisha ya watu kuwa hatarini  kutokana na maji kujaa au kupita kwa kasi

Pia imetoa wito kwa wakazi wa maeneo hayo kuchukua tahadhari stahiki na kuendelea kufuatilia taarifa pamoja na tahadhari zitakazotolewa


Mvua bado ipo ipo sana Mvua bado ipo ipo sana Reviewed by KUSAGANEWS on May 13, 2018 Rating: 5

No comments: