Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango amesema si
rahisi bajeti ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kutowekewa ukomo
Akijibu hoja za wabunge Mei 14, 2018 waliochangia hotuba ya
bajeti ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwa mwaka wa fedha
2018/19, Dk Mpango amesema
“Kuna ushauri ulitolewa wizara isiwekewe ukomo hili si
rahisi, fedha hazitoshelezi yako mahitaji mengi ambayo ni muhimu ambayo ninyi
wabunge mliyasemea kwa nguvu.”
“Mlisema maji, vifaa tiba, kilimo kuwa kwenye mtungi mmoja
lazima uchukue kidogo,” amesema
Dk Mpango amesema Serikali itaendelea kuliwezesha jeshi kwa
kadri rasilimali zinavyoruhusu
Amesema hadi Aprili, 2018 Jeshi la Wananchi wa Tanzania
(JWTZ) lilikuwa limepata fedha za matumizi ya kawaida Sh307.9 bilioni
Waziri Mpango awajibu wabunge bajeti ya Ulinzi
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 14, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment